Lionel Messi atemwa Argentina

Nahodha na Mshambuliaji Lionel Messi atakosa mechi zijazo za Kimataifa ya Kirafiki za Argentina dhidi ya El Salvador na Costa Rica kwa sababu ya jeraha la msuli wa paja la kulia, shirikisho la soka la nchi hiyo limesema.

Nahodha huyo wa Argentina alibadilishwa mapema katika kipindi cha pili cha ushindi wa mabao 3-1 wa wiki iliyopita dhidi ya Nashville kwenye Kombe la Mabingwa wa CONCACAF kwa sababu ya jeraha hilo na alikaa nje ya ushindi wa ligi Jumamosi dhidi ya D.C. United.

Kocha wa Inter Miami CF, Gerardo Tata Martino, alisema baada ya mchezo huo kuwa hali ya Messi itatathminiwa, baada ya wiki.”

Messi mwenye umri wa miaka 36, awali alikuwa amejumuishwa kwenye kikosi cha Argentina kwa mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya El Salvador itakayopigwa Philadelphia kesho Ijumaa (Machi 21), na dhidi ya Costa Rica mjini Los Angeles itakayopigwa Jumanne (Machi 25), lakini hilo limebadilika.

ESPN Argentina iliripoti kwamba Messi bado anaweza kuungana na timu ya taifa baadae wiki hii ili kufanyiwa sehemu ya mchakato wake wa kupona kabla ya kurejea Florida.

Wachezaji kadhaa wa Argentina, akiwamo Mshambuliaji wa Manchester City, Julian Alvarez, waliwasili Philadelphia Jumapili, huku wachezaji wengine wa kikosi walitarajiwa kuungana nao jana Jumanne (Machi 19).

Michezo yote miwili ni ya maandalizi kwa Mabingwa Watetezi, Argentina kwa Copa America Juni na Julai, ambayo pia itakuwa nchini Marekani.

Argentina tayari ilikuwa imewapoteza mshambuliaji Paulo Dybala na kiungo wa kati Exequiel Palaciose kutokana na majeraha.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii