Chad: Mvutano waendelea mwanzoni mwa uchunguzi wa kifo cha mpinzani Yaya Dillo

Nchini Chad, mvutano bado unaendelea kushuhudiwa nchini humo, baada ya kifo cha mmoja wa wapinzani wakuu wa mamlaka ya baba na mwanaye Mahamat Déby, Yaya Dillo mnamo Februari 28, wakati vikosi vya usalama vilipovamia makao makuu ya chama chake, PSF. Serikali inaapa hadi sasa kwamba aliuawa akiwa na silaha mikononi mwake, huku familia yake ikishtumu kile inachoeleza kuwa ni mauaji ya kikatili na kukataa kuomboleza, kama mila inavyoelekeza, kwa kuendelea kudai ukweli.


Familia ya mmoja wa wapinzani wakuu wa utawala wa Mahamat Deby, yaya Dillo inanyooshea kidole cha lawama serikali na vikosi vyake kuhusika kwa mauaji ya kiongozi huyo wa upinzani. Ni katika mazingira haya ambapo jana, Baraza la Kitaifa la Mpito la Chad, lilikutana asubuhi na kupiga kura 103 kuunga mkono azimio la kumuunga mkono rais Mahamat Idriss Déby, na kumpongeza kwa "kufungua uchunguzi ili kutoa mwanga juu ya tukio hili la bahati mbaya la Februari 27 na 28, 2024 ili kubaini wahusika". Uchunguzi ambao bado upo mwanzoni.

Uchunguzi huu ulianza tu mwishoni mwa wiki iliyopita, kulingana na vyanzo vyetu. Mwendesha mashtaka - katika mahakama ya Ndjamena - alikwenda, na timu nzima ya majaji, kwenye koloni ya adhabu ya Koro-Toro kuchunguza ghasia ambazo zilisababisha kifo cha Yaya Dillo mnamo Februari 27 na 28. Kwa mujibu wa chanzo chetu, rais wa mahakama pia alikuwepo.

"Walisikiliza wale wote waliozuiliwa kuhusiana na kesi hii na wanafanyia kazi ripoti yao ambayo itakuwa tayari ndani ya siku mbili," kinaongeza chanzo hiki, ambacho kinataja kuwa "ni wakati huo ambapo "tutajua kinachoendelea kuhusiana na kifo cha Yaya Dillo." Kuhusu uchunguzi kwa ngazi ya "kimataifa" uliotangazwa na Waziri Mkuu, Succès Masra, bado haujaanza, kulingana na chanzo kingine kilicho karibu na kesi hiyo. "Tulilazimika kwanza kujua ni nini hasa kilichotokea, kabla ya kuanzisha uchunguzi wa kimataifa," chanzo hiki kimebaini, kikielezea kuwa katika hatua hii hakuna jambo amalo limeamuliwa au juu ya asili yake au muundo wake. "Lakini kanuni yake imeanzishwa," chanzo hiki kimesisitiza.

Kufikia sasa hakuna mwanga wowote ambao umetolewa kuhusu hali halisi ya kifo cha kiongozi huyo mkuu wa upinzani nchini Chad.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii