Rais Samia Awapongeza Ramadhani Brothers Kwa Kushinda American Got Talent

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewapongeza Wasanii wa sarakasi kutoka Tanzania Ibrahim na Fadhili Ramadhan wanaounda kundi la The Ramadhan Brothers ambao wameibuka Washindi wa mashindano ya kusaka vipaji ya ‘America’s Got Talent Fantasy League’, usiku wa kuamkia leo Nchini Marekani na kujinyakulia $250,000 (Tsh milioni 637.5) pamoja na tuzo ambapo amesema Vijana hao wanaitangaza Tanzania vizuri.

Rais Samia amesema “Pongezi kwa Vijana wetu Fadhili na Ibrahim (The Ramadhani Brothers) kwa kuibuka Washindi katika mashindano ya sanaa na burudani ya AGT: Fantasy League, safari yenu inaendelea kudhihirisha kuwa juhudi, nidhamu, kujituma na kujiamini ni nguzo muhimu kufikia mafanikio, mnaitangaza vyema Nchi yetu na kuweka mfano bora kwa wengine”

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii