Usher Raymond Alilipwa TSH. Milioni 1.7 Kutumbuiza Super Bowl

Kwa mujibu wa taarifa ni kuwa, Usher Raymond alilipwa ($671) sawa na TSh. Milioni 1.7 kutumbuiza kwenye Halftime ya Super Bowl, Jumapili tarehe 11. Kikawaida NFL huwa hawamlipi msanii kufanya onesho hilo, ila huwa wanatoa pesa kiasi kwa ajili ya maandalizi.


Baada ya onesho hilo la dakika 15, Usher anatarajia kutengeneza zaidi ya ($100 million) toka kwenye streaming, mauzo ya tiketi pamoja na dili za udhamini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii