MSANII MASAUTI AELEZA SABABU YA KUKATA NYWELE ZAKE SIO MWANAMKE

Msanii wa muziki kutoka nchini kenya masauti ambaye asili yake ni kutoka Mombasa ni moja kati ya msanii ambaye alifahamika Zaidi katika muonekano wa dread ambazo alikuwa akisuka katika mitindo ya aina tofauti tofauti huku pia akifanikiwa kufanya kazi nyingi nzuri na maarufu za kwake Pamoja na za kushirikishwa na wasanii wengine kutoka kenya nan je ya kenya.

 

 

Kwa sasa masauti ana muonekano tofauti na ule ambao wengi walizoea kumuona nao jambo ambalo limefanya watu wengi waanze kuhoji nini chanzo cha msanii huyo kufanya mabadiliko ya muonekano wake wa nywele kwa kuzikata na kuacha kusuka kulingana na tetesi za mtaani zilidai kuwa msanii huyo ameo mwanamke na hapendi kusuka nywele,lakini baada ya masauti kudakwa na kamera za chanzo kimoja cha muziki nchini kenya alieleza sababu ambayo ni tofauti kidogo na kusema kuwa “hao wanaosema hivyo ni wambea tu mimi ni mtu ambaye nina familia yangu kwahiyo kubadilisha muonekano sijafanya kwaajili ya mwanamkea bali ni kitu ambacho nilikuwa natamani mimi binafsi Pamoja na mama yangu”

Alisema masauti ambaye anakiri kuwa familia yake inafurahia nay eye pia anafurahi kuwa alivyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii