Mamlaka nchini Syria wametangaza siku ya Jumanne kwamba wamekamata kikundi chenye mafungamano na kundi la wanamgambo wa Lebanon, Hezbollah kinachopanga kuwaua maafisa wa serikali.
Mamlaka nchini Syria wametangaza jana Jumanne kwamba wamekamata
kikundi chenye mafungamano na Hezbollah kinachopanga
kuwaua maafisa wa serikali.
Wizara ya mambo ya ndani ya Syria ilisema ilifanya mfululizo wa
operesheni za usalama kwa wakati mmoja katika maeneo ya vijijini ya Damascus,
Aleppo, Homs, Tartus na Latakia.
Ilisema operesheni hizo zilisababisha kubomolewa kwa kikundi
kilichopangwa kinachohusiana na wanamgambo wa Hezbollah, ambao wanachama wake
walijipenyeza katika eneo la Syria baada ya kupata mafunzo maalum nchini
Lebanon.
Aidha taarifa ya wizara hiyo ilisema uchunguzi wa awali ulifichua kwamba kikundi hicho kilikuwa kinapanga mauaji ya kuwalenga maafisa wa ngazi ya juu wa serikali ikiongeza kwamba walikamata vifaa vya kijeshi vikiwemo vifaa vya kulipuka na vifaa vya kufyetulia makombora na maroketi, miongoni mwa silaha zingine.
Ingawa ilichapisha picha za washukiwa 11, bila kutaja uraia wao, ikisema
kwamba walimjumuisha afisa aliyehusika na kupanga na kusimamia mauaji.
Hata hivyo wakati huo huo, Hezbollah ilitoa taarifa ikikanusha kabisa shutuma hizo za uongo kutoka kwa wizara ya mambo ya ndani ya Syria.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime