Rais Volodymyr Zelensky amelaani kile alichokiita kuwa ni ujinga mkubwa wa Urusi kwa kufanya mashambulizi makali huku ikitafuta usitishaji mapigano.
Mashambulizi ya Urusi yamewaua
watu 21 katika miji kote Ukraine huku rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akilaani
kile alichokiita ujinga mkubwa wa Urusi kwa kufanya mashambulizi makali huku
ikitafuta usitishaji mapigano kuandaa gwaride lake la kizalendo Mei 9.
Mashambulizi hayo ya jana Jumanne yaliyoikumba miji ya Zaporizhzhia,
Kramatorsk na Dnipro, yalitokea saa chache kabla ya usitishaji mapigano
uliopendekezwa na Ukraine.
Huko Zaporizhzhia ambao ni mji wa kusini mwa Ukraine ulio karibu na mstari wa mbele wa vita watu 12 waliuawa katika shambulio ambalo Zelensky alilielezea kuwa halina uhalali wowote wa kijeshi.
Mapema
Jumatano, mkuu wa eneo la Crimea ambalo Urusi ililiteka kutoka kwa Ukraine
mnamo mwaka wa 2014 alisema mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Ukraine
yaliwaua raia watano.
Wakati huo huo Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio
alizungumza kwa simu Jumanne na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov,
kulingana na idara ya mambo ya nje.
Hata hivyo msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Tommy Pigott amesema viongozi hao wawili ambao walizungumza kufuatia ombi la Lavrov walijadili uhusiano wa Marekani na Urusi vita vya Urusi na Ukraine na vita vya Iran, bila kutoa maelezo zaidi.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime