Wanamgambo wa RSF waliteka eneo la Babanusa, jimbo la Kordof

Vikosi vya RSF nchini Sudan vimesema, vimechukua udhibiti kamili wa eneo muhimu la Babanusa, linalotumika pakubwa kwa usafirishaji kusini mwa nchi hiyo kuliko na utajiri wa mafuta.


Katika taarifa yao, wanamgambo hao wamesema utekaji wa eneo hilo lililoko katika jimbo la Kordofan Magharibi, umefanyika wakati walipokuwa wakizuia shambulizi la kushtukiza kutoka kwa jeshi la Sudan, katika kile walichokiita, "ukiukaji wa wazi wa amri ya kusitisha mapigano kwa ajili ya utoaji wa misaada.

Uvamizi huo wa Babanusa uliofanywa na RSF ni mwendelezo wa wanamgambo hao baada ya kuliteka eneo la El-Fasher huko Darfur mnamo mwezi wa Oktoba.

Mnamo Novemba 19, Rais wa Marekani Donald Trump alisema ataingilia kati kusitisha vita hivyo vilivyoanza Aprili 2023.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii