Katika kuendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya kijamii ili kudumisha amani na kuimarisha usalama pamoja na kudhibiti matukio mbalimbali ya kihalifu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi DCP-Wilbrod Mutafungwa leo Disemba 1.2025 amefanya kikao na Maafisa usafirishaji (Bodaboda) wa kanda ya Kishiri, kata ya Kishiri Wilaya ya Nyamagana. Ambapo amewasisitiza kudumisha amani iliyopo ili kutoa nafasi kwa viongozi walioko madarakani kupata nafasi ya kuweza kuleta maendeo kwani maendeleo hayawezi kuja kwenye fujo.
"Sisi kama wananchi wa Mkoa wa Mwanza tunayo nafasi kubwa ya kudumisha amani iliyopo kamwe tusishiriki kwenye matukio ya uvunjifu wa amani, tusiruhusu kamwe matendo ya fujo, uporaji, maandama yasiokuwa halali ambapo mambo yaho yote yatadhorotesha maendeleo"
Aidha, Kamanda Mutafungwa amewataka mafisa hao kufichua uhalifu kwa kutoa taarifa kwa Vyombo husika hususan Jeshi la Polisi ili liweze kuchukuwa hatua kwani Nchi yetu inaongozwa kwa mujibu wa sheria.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya maadili kanda ya Kishiri James Simon amewataka Jeshi la Polisi kutoa imani kwa maafisa usafirishaji katika kudumisha amani na wako tayari kutoa taarifa za matukio ya kihalifu.
Vilevie Afisa usafirishaji (Bodaboda) ameahidi kwa Jeshi la Polisi kupitia ushirikiano unaotolewa baina yao na wananchi kwa ajili ya kuimarisha amani ya Taifa letu kwani hawatawangusha na kuahidi kutembea kituo hadi kituo kwa ajili ya kutoa elimu ya kudumisha amani.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime