Rais wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan, azindua rasmi daraja la JP Magufuli Jijini Mwanza

Rais Samia Suluhu Hassan leo, Alhamisi Juni 19, 2025 amezindua Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) jijini Mwanza lenye urefu wa kilometa 3.0 na barabara unganishi yenye urefu wa kilometa 1.66.

Miongoni mwa wageni waliohudhuria uzinduzi huo ni mjane wa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, Mama Janeth Magufuli ambapo daraja hilo lenye ulefu wa Km 3, limeunganisha Kigongo (wilaya ya Misungwi, Mkoa wa Mwanza) na Busisi (wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Geita) kwenye Ziwa Victoria.

Ujenzi wa daraja hilo uliasisiwa na Hayati Magufuli  aliyefariki Machi 17, 2021 likiwa limefikia asilimia 24.6 za utekelezwaji wake na mrithi wake, Rais Samia Suluhu Hassan aliendeleza na hatimaye kukamilisha.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii