Bunge laja na mswaada wa sheria kwa wapangaji wa serikali kulipa bill sawa na wapangaji wangine

Bungeni leo Juni 9, 2025 limepitisha Muswada wa wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Shirika la Nyumba la Taifa wa Mwaka 2025 (The National Housing Corporation (Amendment) Bill 2025).

Muswada huo uliwasilishwa mapema leo asubuhi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi na kusema kuwa miongoni mwa marekebisho yanayopendekezwa ni kuhusu mamlaka ya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa shirika.

Kifungu cha 18 kinapendekezwa kurekebishwa kwa kuweka mamlaka ya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu kuwa ni Rais badala ya Waziri pamoja na kuboresha masharti ya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika. Lengo la marekebisho haya ni kuimarisha utawala bora na uwajibikaji katika usimamizi wa Shirika.

Aidha kifungu kipya cha 18A kinapendekezwa kuongezwa ili kutenganisha masharti yanayohusu uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika na ajira za maafisa na wafanyakazi wengine wa Shirika.

Lengo la marekebisho haya ni kuweka mpangilio bora wa masharti ya sheria kwa kuzingatia misingi ya uandishi wa sheria .

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii