Rais Samia Awasili Addis Ababa Kushiriki Mkutano Wa 38 Wa AU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili leo, tarehe 14 Februari 2025, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, Addis Ababa, nchini Ethiopia, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).

Katika mkutano huu wa muhimu, Mhe. Rais Dkt. Samia atakuwa sehemu ya majadiliano ya kimataifa kuhusu masuala mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa, na kijamii, huku akihusishwa pia na mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika.

Mkutano huu ni fursa muhimu kwa viongozi wa Afrika kuzungumzia changamoto zinazoukumba bara hili na kutafuta suluhisho za pamoja, huku Tanzania ikionyesha uongozi wake katika juhudi za kudumisha amani, usalama, na maendeleo ya kiuchumi katika ukanda wa Afrika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii