Polisi "Faini Milioni 5 Mpaka 20 Ukibainika Kupekua Simu ya Mwenza Wako"

Mkuu wa Polisi wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Selestin Luhende amewataka wanandoa kuacha kupekua simu za wenza wao ili kuepuka madhara yanayoweza kupatikana ikiwemo ugomvi unaoweza kuvunja ndoa pamoja na adhabu zinazoweza kutolewa kwa mujibu wa sheria.


Amesema pia endapo mwanandoa utabainika au kukutwa na hatia ya kupekua simu ya mwenza wako adhabu yake kwa mujibu wa sheria ni faini ya Milioni tano mpaka Milioni ishirini au kifungo cha miaka mitano na wakati mwingine vyote kwa pamoja.


Luhende ameeleza hayo wakati akitoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya usalama katika kikao cha baraza la madiwani kilichokuwa kikiendelea wilayani humo.


"Kupekua simu ya mwenza wako au kuangalia meseji zilizoandikwa ujue tayari umevunja sheria za nchi na ukipatikana na hatia adhabu yake ni Shilingi Milioni tano au Milioni Ishirini au kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja"amesema OCD Selestin Luhende


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii