Putin afanya mabadiliko safu ya ulinzi

Rais wa Urusi, Vladimir Putin amefanya mabadiliko na kumuondoa Waziri wa ulinzi, lkjaziri Sergei Shoigu ikiwa ni sehemu ya kupanga safu yake wakati huu anapoanza awamu yake ya tano madarakani.

Shoigu hata hivyo ameteuliwa kuwa katibu wa Baraza la Usalama la Urusi, na nafasi yake kuchukuliwa na Andrei Belousov ambaye alikuwa Naibu Waziri Mkuu anayedaiwa kubobea katika masuala ya uchumi.

Baraza lote la Mawaziri lilijiuzulu Mei 7, 2024 baada ya kuapishwa kwa Putin japo mawaziri wengi walitarajiwa kubaki katika nafasi zao.

Shoigu aliteuliwa kuwa Waziri wa ulinzi mwaka 2012, ikiwa ni miaka miwili kabla ya Urusi kulinyakua jimbo la Ukraine la Crimea.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii