Mashabiki Nigeria Waisusa Show ya Davido, Waingia Mashabiki Wasio zidi 100 tu

Show msanii mkubwa kutoka nchini Nigeria @davido leo hii pale Eagle square Abuja nchini Nigeria imewashangaza wengi akiwemo Davido mwenyewe baada ya mashabiki kuisusia na kushindwa kujitokeza kwa wingi kama ilivyozoeleka.

Abuja ni mji mkuu wa nchi ya Nigeria kama ilivyo Dodoma kwa Tanzania,kwa mujibu wa mashuhuda waliofika kwenye eneo la tukio wanadai kuwa mashabiki waliojitokeza hawajafika hata mia moja(100).

@davido ameshangazwa na tukio hilo na kuhisi pengine watu wanamfanyia prank lakini huo ndio uhalisia,unahisi kwanini mashabiki wameshindwa kujitokeza kwa wingi kwenye show ya gwiji huyo wa muziki wa Afrobeats.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii