Rais Samia Aongeza Mzuka Taifa Stars

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Adel Amrouche amesema kitendo cha Rais Samia Suluhu Hassan kutoa ndege kwa ajili ya timu hiyo kinawapa ari ya kupambana zaidi ili kupata matokeo katika michezo iliyo mbeleni.


Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini Morocco tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Niger, kocha huyo amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuunga mkono michezo na kwamba wanajihisi wenye deni na wapo tayari kuipeperusha vyema bendera ya taifa katika michezo yao.


Stars inaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Grand Marrakech Annex1 wakisubiri kuivaa Niger katika mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu kombe la dunia 2026 mwaka utakaopigwa mjini Marrakech Morocco Novemba, 18,2023.


Ndege iliyotolewa na Rais Samia itaisubiri timu hiyo ili kuirudisha nyumbani mapema kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa pili dhidi ya Morocco utakaopigwa Novemba 21 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii