Madaraja ya mpaka wa Canada, na Marekani yahofia mlipuko

Madaraja yote manne ya mpaka wa Marekani, na Canada, magharibi mwa New York yalifungwa Jumatano mchana baada ya kuripotiwa mlipuko wa gari kwenye daraja la Rainbow karibu na maporomoko ya maji ya Niagara, na kuziweka nchi zote mbili katika hali ya tahadhari.


Gavana wa New York Kathy Hochul aliwambia waan dishi habari kwamba hakuna ishara kwamba hilo lilikua shambulio la kigaidi, lakini uchunguzi ungali unaendelea.


White House imesema rais Joe Biden wa Marekani, aliataarifiwa kuhusu tukio hilo, huku waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau, akiliambia bunge kuwa hali ni mbaya katika Maporomoko ya maji ya Niagara.


Waziri mkuu Trudeau, alijiondoa katika kipindi cha maswali katika bunge ili afahamishwe zaidi kuhusu tukio hilo, na alisema kwamba wamelichukulia kwa uzito wa kipekee.


Mlipuko huo ulitokea upande wa Marekani wa daraja la Rainbow, linalounganisha nchi hizo mbili juu ya mto Niagara.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii