Marekani yamuwekea vikwazo mfanyabiashara wa silaha wa Russia

Marekani, Jumatano imewaweka maafisa wa biashara wenye uhusiano na  vita vya Russia dhidi ya Ukraine katika orodha ya vikwazo.

Orodha hiyo inamjumuisha mlanguzi wa silaha Igor Zimenkov, mtoto wake wa kiume, na kundi la makampuni aliyo na ubia ya Asia, Ulaya, na mashariki ya kati kwa kuisaidia Moscow kupata silaha zaidi kwa ajili ya mapigano yake ya mwaka mzima.

Wizara ya fedha ya Marekani imeweka vikwazo dhidi mfanyabiashara wa silaha wa Russia Zimenkov, mtoto wake wa kiume Jonatan, na makampuni yenye uhusiano na Zimenkov ya Singapore, Cyprus, Bulgaria, na Israel pamoja na mataifa mengine.

Wizara ya fedha imewataja watu 22 na taasisi ambazo zimehusishwa na vikwazo na mtandao wa viwanda vya kijeshi vya Russia.

Katika kipindi cha mwaka jana, wizara imesema imewawekea vikwazo watu 100 na taasisi zinazo jihusisha na shughuli ambazo zimewekewa vikwazo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii