Mwekezaji adaiwa kulazimisha wananchi wauze nyumba

Wananchi wa mtaa wa Migombani, Kata ya Mitimirefu Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamedai kulazimishwa kuuza nyumba zao kwa bei isiyoendana na thamani ya nyumba husika ili kumpisha mwekezaji aliyeweka bandari kavu katika eneo hilo.

Wananchi hao  wamesema mwekezaji huyo amekuwa akiwafanyia tathmini yeye mwenyewe bila kuangalia thamani na gharama ya nyumba huku wakidai amekuwa akitumia maneno ya kebehi na vitisho dhidi yao.


Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati iliyoundwa  kwa ajili ya kutetea wananchi katika eneo hilo la Migombani Chumu Samwel, amesema eneo hilo ambalo lina wakazi zaidi ya elfu moja baadhi yao wameondolewa kwa kupewa fedha ambazo si stahiki kwao huku mwekezaji akiendelea kuweka makontena kwenye eneo la makazi ya watu licha ya wananchi kugoma kuuza nyumba zao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii