Serikali yatoa neno Mtanzania aliyefia Urusi

aziri wa Mambo ya Nje Dkt. Stergomena Tax, amesema Mtanzania aliyefariki dunia nchini Urusi Nemes Tarimo, alikuwepo nchini humo kwa ajili ya masomo na alijiunga na chuo cha Moscow Technology Pro mwaka 2020 kwa masomo ya shahada ya uzamili katika fani ya Business Informatics.

Waziri amesema taarifa walizozipokea ni kwamba mwezi Machi 2022 Mtanzania huyo alikuhumiwa kifungo cha miaka saba gerezani kwa mujibu wa sheria za Urusi kwa vitendo vya uhalifu 

Na kwamba akiwa gerezani alipewa nafasi ya kujiunga na kikundi cha kijeshi kilichopo nchini humo kinachofahamika kama Wagner kwa ahadi ya kulipwa fedha lakini pia kwa ahadi ya kuachiwa huru mara baada ya vita na alikubali kujiunga na kikundi hicho 

Hata hivyo Waziri Dkt. Tax ameeleza kuwa mwili wa marehemu unawasili leo ingawaje serikali haitahusika na masuala yoyote ya mazishi yake.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii