Serikali Kuchunguza Vitabu vya Watoto Vinavyofundisha Ushoga

Serikali imesema inafuatilia suala la vitabu vya shule vinavyodaiwa kuwa na maudhui ya kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja kwa watoto na kutoa taarifa rasmi.

Hatua hiyo imekuja baada ya kusambaa kwa picha za vitabu hivyo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kusababisha taharuki kubwa kwa wazazi hapa nchini.

Akizungumza Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amesema hakuna taasisi yoyote yenye mamlaka ya kusambaza au kutumia vitabu bila kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).

“Tutafanya uchunguzi kuangalia ukweli wake halafu tutatoa kauli, lakini vitabu vyote vinavyotumika hapa nchini ni vile vilivyopata ithibati kutoka kwa Kamishna wa Elimu Tanzania na TET. TET ndiyo inaratibu vitabu vyote vya kujifunzia yaani kiada na ziada,” ameeleza.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii