Mawaziri Wa Kenya Warushiana Maneno Na Wanachi Wa kenya

Mawaziri wa serikali ya Rais William Ruto wanaonekana kukosa mwelekeo kuhusu masuala kadhaa na kuishia kujibizana kwenye umma.
Kwa sasa suala la uagizaji wa mahindi kutoka nje limeonekana kugawanya baraza la mawaziri huku Waziri wa Biashara Moses Kuria akitupwa kikaangoni.Kuria alikuwa amesema serikali itaagiza mahindi yanayozalishwa na teknolojia ya kisayansi maarufu kama GMO kutokana na uhaba wa mahindi nchini.
Lakini sasa mawaziri wengine wamejitenga na Kuria wakisema hawajui alitoa wapi ripoti alizopeana
Akiongea Jumatatu Novemba 28 na kamati ya magavana nchini, Waziri wa Kilimo Mithika Linturi alisema wizara yake haina ripoti za uhaba wa mahindi nchini.
"Kuweni wapole mtakuwa na chakula cha kutosha. Mimi ndio nasimamia mambo ya chakula humu nchini na nitatoa ripoti kamili mara tu nikipata deta yote," alisema Mithika.
Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi alikuwa pia amepuuza Kuria akisema mambo ya chakula yana waziri wake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii