UKOSEFU WA ELIMU VIMETAJWA KUWA NI SABABU YA KUWEPO KWA VITENDO VYA UKATILI

MILA na desturi na ukosefu wa elimu vimetajwa kuwa sababu ya kuwepo kwavitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii kwa watoto ikiwa ni pamoja nakuendelea kuwepo kwa vitendo vya ukeketaji kwa watoto wadogo.
Sababu hizo zimetolewa na wananchi wa Wilaya ya Singida na Iikungi wakati
Taasisi ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania –( SMAUJATA)  wakito elimu ya kupinga vitendo vya ukatiliwa kijinsia kwa akina mama wajawazito katika Hosiptal ya Makiungu wilayani Ikungi.
Wamesema kuwa kuna baadhi ya wananchi bado wanaendelea kufuata mila nadesturi zilizopitwa na wakati ambazo bado zinasababisha kufanyika kwa vitendohivyo vya ukatili.
Wameongeza kuwa hata mangariba wamebadili njia ya kufanya ukeketaji ambapokwa sasa vitendo vya ukeketaji unafanywa kwa watoto wachanga .
Kutokana na sababu hizo, taasisi ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamiitanzania – SMAUJATA imeitembelea hospital ya makiungu wilayani ikungi  mkoani singida kutoa elimu ya kupambana naukatili wa kijinsia hasa vitendo vya ukeketaji kwa watoto kwa akina mama wajawazito.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Singida Dismas Kombe, alisema wanatoa elimukwa akina mama wajawazito kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutambua ubaya waukatili wa kijinsia ili waweze kuwalinda watoto wao wanaotarajia kuwaza navitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia.
Kombe alisema kuwa bado makundi la watoto na wanawake yanafanyiwa vitendovya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na ukeketaji kwa watoto, vipigo naubakwaji katika maeneo mbalimbali nchini.
Kombe ameongeza pia changamoto iliyopo kwa jamii ni kushindwa kuripotivitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa akina mama na watoto, kutokanana vitendo vingi kufanywa na wanandugu.
Katibu idara ya wanaume SMAUJATA – Mkoa Singida, Simon  Mdumah alisema kundi la wanaume nalo ni mojaya kundi linalofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa sasa, changamoto ninamna ya wanaume hao kuripoti vitendo hivyo wanavyofanyiwa.
Mdumah alisema wanaume wengi wanashindwa kuripoti ukatili wanaofanyiwakutokana na mila na desturi za kiafrika na kuogopa kuonekana wadhaifu kwa wakezao na jamii kwa ujumla.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii