Mlipuko wa Polio Indonesia, wanaopinga chanjo wanasema ina pombe na nyama ya nguruwe

Indonesia imeanza kutoa chanjo dhidi ya polio katika mikoa yenye watu wenye sera za kihafidhina, baada ya watu wanne kugunduliwa kuambukizwa ugonjwa huo hatari na uliotangazwa kwamba umetokomezwa kote duniani karibu mwongo mmoja uliopita.

Maambukizi yaligunduliwa mwezi Oktoba, katika mvulana mwenye umri wa miaka 7 na watu wengine watatu wamethibitishwa kuambukizwa.

Kampeni ya kutoa chanjo ilianza jana Jumatatu na inalenga Watoto milioni 1.2.

Kampeni hiyo hata hivyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya habari potofu kwamba chanjo inayotolewa ina pombe na imetengenezwa kutoka kwa nyama ya nguruwe, vitu viwili ambavyo haviruhusiwi kabisa katika dini ya kiislamu.

Serikali ya Indonesia imekuwa ikizingatia zaidi chanjo dhidi ya virusi vya Corona.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii