Wakenya Washtakiwa Marekani Kwa Utapeli

Raia wa Somalia wenye uhusiano na Kenya ni miongoni mwa washukiwa 47 walioshtakiwa nchini Marekani kwa utapeli.

Raia hao wanaoishi Marekani, wanatuhumiwa kuiba KSh25 bilioni zilizokusudiwa kuwasaidia watoto wakati wa janga la corona.

Marekani ilitangaza Jumatano, Septemba 21, kwamba washukiwa hao wanahusishwa na Aimee Bock ambaye ni mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa Feeding Our Future,ambalo lilikuwa limeshirikiana na Marekani kutoa msaada wa chakula kwa watoto jimboni Minnesota.

Wasomali hao wanadaiwa kushirikiana na wafanyakazi wa ‘Feeding Our Future’kufungua tovuti feki ambazo walitumia kupata mabilioni za pesa kutoka kwa serikali ya jimbo la Minnesota.

Kwa mujibu wa mashtaka, Aimee Bock anaripotiwa kushirikiana na matepeli hao kufungua tovuti 250 feki zikidai kulisha maelfu ya watoto jimboni humo kwa siku ndani ya siku chache au wiki baada ya kuundwa.

Idara ya Haki (DoJ) katika taarifa ilisema kuwa washukiwa hao hawakutumia pesa hizo kuwalisha watoto badala yake walizitumia kununua magari na majumba ya kifahari katika majimbo ya Minnesota, Ohio na Kentucky.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii