Korea Kaskazini yafyatua kombora

Korea Kaskazini leo imefyetua kombora la masafa marefu kuelekea baharini mashariki mwa Pwani yake . Haya ni kwa mujibu wa viongozi wakuu wa kijeshi wa Korea Kusini kabla ya mazoezi makubwa ya kijeshi yaliyopangwa kufanywa na vikosi vya Korea Kusini na Marekani.Shirika la habari la Yonhap nchini Korea Kusini, limeripoti jana kuwa huenda Korea Kaskazini inajiandaa kufanya jaribio la kombora linalorushwa kutoka kwenye nyambizi, SLBM, hayo yakiwa ni kulingana na jeshi la Korea Kusini.

Kurushwa kwa kombora hilo, kunakuja baada ya kuwasili kwa meli ya kivita yenye eneo la kupaa na kutua kwa ndege ya Marekani nchini Korea Kusini na kabla ya ziara iliyopangwa wiki ijayo ya makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris. Jeshi la Korea Kusini halikutoa maelezo zaidi kuhusu kombora hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii