Man United yamtambua aliyepanda na bendera Kilimanjaro

Shabiki wa Man United Martin Hibbert (45) ametimiza ndoto yake ya kupanda mlima Kilimanjaro akiwa na wheel chair (kiti cha matairi) baada ya kupooza 2017 kufuatia shambulio la bomu lililopigwa May 22 2017 Manchester Arena muda mchache baada ya tamasha la msanii Ariana Grande.


Hibbert ambaye aliambiwa kuwa hawezi tena kutembea kutokana na shambulio hilo kumsababishia tatizo katika uti wa mgongo, ameamua kupanda hadi kileleni kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia watu wenye tatizo la uti wa mgongo pamoja na kuwatia moyo kuwa walemavu wanaweza.

“Watu wenye ulemavu wana uwezo wa kufanya chochote wanachotaka kufanya, natumaini watu wanaona hilo na kusapoti walio na ulemavu na kutowarudisha nyuma”>>> Martin Habbert

Taarifa ya Martin Hibbert imechapishwa na mitandao mbalimbali UK ikiwemo tovuti na page rasmi za Man United, hadi sasa Hibbert amechangisha pound 50,000 (Tsh milioni 141) na lengo lake ni kufikisha jumla ya pound milioni 1 (Tsh Bilioni 2.8).

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii